
ZOEZI LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Leo, tarehe 27 Novemba 2024, wananchi wa Tanzania walijumuika kwa wingi katika zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, linalohusisha uteuzi wa viongozi wa ngazi za chini za utawala, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji. Uchaguzi huu ni muhimu katika kuimarisha demokrasia na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za utawala wa maeneo yao.
Katika tukio hili la kihistoria, wafanyakazi wa STAMIGOLD, wakiongozwa na Meneja Mkuu wa Mgodi (Bw. Ali.S.Ali) walijumuika wote pamoja na wananchi wa mavota kwa pamoja kwenye zoezi la kupiga kura, Katika Kituo cha KALAMATA kilichopo Kata ya Kaniha, Kijiji cha Mavota, Wilaya ya Biharamulo.
Aidha, zoezi hili la uchaguzi limekuwa na mafanikio makubwa, huku wananchi wakionyesha ujasiri na utayari katika kuchagua viongozi waaminifu na wenye uwezo wa kuleta maendeleo katika vijiji vyao. Kwa ujumla, uchaguzi wa leo umeendelea kuwa na amani na utulivu, ambapo kila mchakato umeendeshwa kwa usahihi na kwa kufuata sheria na taratibu za uchaguzi zilizowekwa.
Wafanyakazi wa STAMIGOLD walionesha mshikamano wa kipekee katika zoezi hili, huku wengi wakijivunia kujumuika katika kuchagua viongozi watakaowafaa katika nafasi hizo muhimu. Uchaguzi huu umeendelea kuwa ishara ya kuimarika kwa demokrasia na ushirikiano kati ya Serikali na wananchi katika ngazi ya Kijiji, ambapo uongozi mzuri ni msingi wa maendeleo endelevu.
“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni njia mojawapo ya kuimarisha demokrasia na ushirikiano kati ya wananchi na viongozi wao. Kama STAMIGOLD, tunajivunia kuwa sehemu ya jamii na tutaendelea kuchangia maendeleo ya maeneo tunayofanyia kazi,"